Violezo vya CV

Violezo vitatu vya bure vya Word. Pakua, jaza kwa maelezo yako, na utume.

Wasifu (CV) mzuri ni mfupi, wazi na wa kweli. Violezo hivi vina mpangilio tayari; unabadilisha maneno yaliyo ndani yake kwa maelezo yako.

Kila kiolezo ni faili la Word (.docx) linalofunguka kwenye Microsoft Word, Google Docs na LibreOffice.

  • Wasifu wa kawaida

    Kwa wengi wanaoomba kazi ofisini, dukani au huduma kwa wateja.

    Kichwa chenye jina na mawasiliano, muhtasari mfupi, uzoefu wa kazi, elimu, ujuzi na wadhamini.

    Faili la Word (.docx), lenye maelezo ya kujaza kwenye mabano [ ]

  • Wasifu wa kazi ya kwanza

    Kwa wahitimu na wasio na uzoefu wa kazi bado.

    Elimu na ujuzi mwanzoni, kisha mafunzo kwa vitendo, kazi za kujitolea na shughuli nyingine.

    Faili la Word (.docx), lenye maelezo ya kujaza kwenye mabano [ ]

  • Wasifu unaoonyesha ujuzi

    Kwa fundi, dereva, mhudumu na kazi za mikono ambapo ujuzi unaonekana zaidi ya vyeo.

    Ujuzi na vyeti mwanzoni, kisha mahali ulipofanya kazi na wadhamini.

    Faili la Word (.docx), lenye maelezo ya kujaza kwenye mabano [ ]

Tengeneza CV kwenye programu ya Nafasi

Programu ya Nafasi ina zana ya kutengeneza CV hatua kwa hatua, na unaweza kutuma ombi la kazi ukiwa nayo.

Pata programu ya Nafasi

Unahitaji barua ya maombi pamoja na CV? Andika barua ya maombi ya kazi

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara